Maafisa wa Israel na wapiganaji wa Hamas, walitangaza Jumanne kwamba wamekubaliana juu ya usitishaji mapigano wa siku nne ili kuwezesha kundi la wanamgambo kuwaachia huru mateka 50 kati ya karibu 200 wanaoshikiliwa.
Baraza la mawaziri la waziri mkuu Benjamin Netanyahu lilidhinisha makubaliano hayo baada ya majadiliano ya karibu usiku mzima ambapo mawaziri walokua wanapinga makubaliano hayo walisema huu ulikua ni uwamuzi mgumu lakini ni uwamuzi ulo sahihi.
Viongozi wa Dunia wapongeza Makubaliano
Rais Biden amesema “nimefurahishwa kupita kiasi kwamba baadhi ya watu hawa hodari wataungana tena na familia zao mara tu makaubaliano yatatekelezwa kikamilifu.”
China, Ujerumani, Ufaransa zimekua nchi za kwanza kupongeza makubaliano hayo yaliyofikiwa kutokana na upatanishi wa Qatar.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Mao Ning amesema usitishaji huo wa muda utasaidia kupunguza janga la kibinadamu, kupunguza mvutano, na kupunguza mashambulizi.
Maskubaliano yaliyofikiwa
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Qatar iliyotolewa Jumatano asubuhi imethibitisha kufikiwa kwa makubaliano, ikisema wakati wa kuanza kusitishwa kwa muda mapigano utatangazwa katika muda was aa 24 zijazo na kudumu kwa siku nne, na kuweza kuongezwa.
Msemaji wa serikali ya Israel amesema kwamba chini ya makubalino hayo karibu mateka 50 wa Isreal na wa kigeni wataachiwa huru hasa wanawake na watoto , ili nayo Israel isitishe mashambulizi ya kijeshi kwa siku nne.
Baada ya hapo matekwa 10 wataachili huru kwa usitishaji mapigano kwa siku moja.
Hamas ilitoa taarifa kupongeza makubaliano hayo ya usitishaji wa muda kwa ajili ya ubinadamu na kwa upande mwengine Israel itawaachilia huru wapalestina 150 wanoashikiliwa katika jela za Israel. Usitishaji huo unawapatia pia wakazi wa Gaza afweni kidogo kuweza kupumzika kutokana na wiki saba za mashambulizi.
Ripoti hii imetayarishwa kutokana na habari kutoka AFP na Reuters
Forum