Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 14:36

Israel imeanza mashambulio kusini mwa Gaza licha ya wito wa kimataifa kusitisha mapigano


Wapalestina waonekana wakilia baada ya jeshi la Israeli kushambulia hospitali ya Nasser mjini Khan Younis
Wapalestina waonekana wakilia baada ya jeshi la Israeli kushambulia hospitali ya Nasser mjini Khan Younis

Utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani unaishinikiza Israel kuchukua tahadhari kuzuia mauwaji ya raia wa Palestina wakati mapigano mapya yameanza Juujmapili kati kati ya Ukanda wa Gaza.

Mji wa Khan Yunis upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza umeshambuliwa kwa mfululizo wa mabomu kutoka jeshi la Israel tangu kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda siku ya Ijuma kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Kulingana na shirika la habari la Associate Press, Israel imetoa onyo kwa wakazi wa kusini mwa gaza kuhama baada ya kukimbia kutoka maeneo ya kaskazini, inapobadili mkakati wake wa mashambulizi kuelekea upande wa kusini, ambako inadai viongozi wa Hamas wamejificha.

Watu wanaojaribu kukimbia kutoka Ukanda wa Gaza wasubiri kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah upande wa Misri.
Watu wanaojaribu kukimbia kutoka Ukanda wa Gaza wasubiri kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah upande wa Misri.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jumamosui kwamba kampeni ya mashambulizi itaendelea hadi mateka walochukuliwa na Hamas hapo Oktoba 7 wamerudishwa na kundi la Hamas limeangamizwa.

“Vita vikali vitarajiwe siku za mbele,” alisema Netanyahu.

Makamu rais wa Marekani, Kamala Harris alisema Jumamosi kwamba “Wapalestina wengi wasio na hatia wameuliwa.” Akizungumza kwenye mkutano wa hali ya hewa COP 28 mjini Dubai, amesema “kwa hakika kiwango cha maafa kikachowakumba raia na picha na video kutoka Gaza ni za kusikitisha sana.”

Karibu wapalestina 200 wameuliwa tangu kuvunjika kwa makubaliano kati ya Hamas na Israel siku ya Ijuma, na hivo kuongeza kiwango cha vifo kufikia 15 523 tangu kuanza mapigano ya Oktoba huko Gaza kulingana na wizara ya afya ya Gaza na watu wengine elfu 40 wamejeruhiwa, na kwamba asili mia 70 kati yao ni wanawake na watoto.

Forum

XS
SM
MD
LG