Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:41

Wapiganaji wa Tigray wakanusha madai ya jeshi la Ethiopia


Dina Mufti
Dina Mufti

Ethiopia imesema Alhamisi vikosi vya waasi kutoka eneo la Tigray vilishindwa katika mkoa jirani wa Afar na vilikuwa vimeondoka.

Lakini vikosi vya Tigray vimesema walikuwa wamehamisha tu wanajeshi kwenda eneo jirani la Amhara kwa mashambulizi huko.

Kikosi cha TPLF, kimeondoka mkoa wa Afar, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ethiopia, Dina Mufti, aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano mjini Addis Ababa.

Kulingana na habari za jeshi, walishindwa na wakaondoka, alisema.

Msemaji wa Tigray, Getachew Reda, akizungumza na shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kutoka eneo ambalo halijafahamika alisema viongozi wa Ethiopia walikuwa wamegundua sasa kuwa vikosi vya Tigray vimeondoka.

"Hatukushindwa. Hakukuwa na mapigano huko Afar, kwa hivyo tulihamisha wanajeshi kutoka huko hadi nyanda za juu zilizo karibu na mkoa wa Amhara," alisema Reda.

vyanzo vya habari vinaeleza kuwa haikuwezekana mara moja kuthibitisha madai hayo.

Wasemaji wa jeshi la Ethiopia na ofisi ya Waziri Mkuu hawakuweza kufikiwa mara moja kutoa maoni juu ya maelezo ya Tigray kuhusu matukio hayo.

XS
SM
MD
LG