Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:34

Guterres aonya kuhusu mzozo wa Ethiopia


Katibu mkuu wa Umoja wa Matafa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Matafa Antonio Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonia Guterres Alhamisi alilieleza baraza la usalama la Umoja huo kwamba mzozo wa Ethiopia umeenea na kuvuka mipaka ya jimbo la kaskazini la Tigray na kwamba, “janga la kibinadamu linajitokeza mbele ya macho yetu."

Ethiopia inakumbwa na mzozo uliozuka miezi tisa iliyopita na ambao umeenea kwenye maeneo mengine.Serikali imeshindwa kudhibiti milipuko mingine ya ghasia za kikabila na kisiasa kuhusu umiliki wa ardhi na rasilimali.

Watu wenye silaha waliua watu 150 wiki iliyopita kaskazini mwa Ethiopia katika shambulio la kundi lenye silaha, tume ya serikali ya haki za binadamu imesema Alhamisi.

“Kauli za uchochezi na kuweka mbele ukabila vinasambaratisha jamii”, Guterres ameliambia baraza la usalama la Umoja wa mataifa lenye wanachama 15.

Ameongeza kuwa “ pande zote lazima zimalize uhasama bila masharti yoyote na kutumia fursa hiyo kujadili sitisho la mapigano la kudumu."

Guterres amesema zaidi ya watu millioni 2 walihamishwa kwenye makazi yao katika mzozo huo na mamilioni ya wengine wanahitaji msaada, ikiwemo chakula, maji, makao, na huduma za afya.

XS
SM
MD
LG