Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:46

UN yatoa wito wa kusitishwa uhasama na mapigano Tigray


Katibu Mkuu Antonio Guterres
Katibu Mkuu Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kusitishwa uhasama na mapigano maramoja katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray.

Guterres amesema kuna haja ya kuwepo na mazungumzo yatakayo ongozwa na Ethiopia ili kumaliza mzozo huo.

Akizungumza na waandishi habari mjini New York Alhamisi, amesema wakati umefika kwa pande zote kutambua hakuna suluhisho la kijeshi litakaloweza kumaliza mzozo huo.

Katibu mkuu amesema kwamba kuenea kwa mapigano kumewatumbukiza watu katika hali mbaya zaidio ya kutisha.

"Watu wa Ethiopia wametaabika sana. Hali ya kibinadamu ni sawa na kuishi motoni. Mamilioni ya watu wanahitaji msaada, miundombinu imeharibiwa na tumesikia moja kwa moja juu ya matatizo yanayowakumba wanawake wanaokabiliwa na ghasia zisizoweza kutajwa. Na kuenea kwa mgogoro kumewasababisha watu kuishi kwa hofu zaidi," ameeleza Guterres.

Katibu mkuu anasema amezungumza na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mapema Alhamisi na kwamba aliahidi mambo yatakuwa mazuri zaidi lakini anasema inabidi kuona kile kitakachofanyika mnamo siku chache zijazo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Ahadi zilizotolewa awali hazijatekelezwa ili kuruhusu msaada wa dharura kuingia Tigray bila pingamizi kama vile UN unataka ili kuweza kuwafikia karibu watu milioni 6 katika jimbo la Tigray.

Kulingana na taarifa ya UN juu ya hali ya kibinadamu huko Tigray iliyotolewa jana ni kwamba kuna karibu malori 100 yenye bidhaa za dharura ambapo 90 yamesheheni chakula yanabidi kuingia Tigray kila siku ili kiuwahudumia karibu watu milioni 5 wenye mahitaji ya dharura. Lakini taarifa inasema hadi sasa ni malori 316 yaliyoweza kuingia kati ya tarehe 12 Julai hadi kufikia jumapili iliyopita.

Katibu Mkuu Gutderres hivyo basi amehimiza kubuniwa hali itakayoruhusu kuwepo na mazungumzo yatakayongozwa na Waethiopia wenyewe na kuruhusu msaada kufikishwa.

Antonio Guterres : "Wakati umefika kwa pande zote kutambua kwamba hakuna suluhisho la kijeshi na ni muhimu sana kuhifadhi umoja na utulivu wa Ethiopia ambayo ni nyeti kwa kanda zikma. Ili kupatia amani nafasi, mimi ninatoa wito wa hatua kuchukuliwa katika nyanja tatu. Kusitisha uhasama, kuruhusu msaada kuingia bila pingamizi na tatu kubuni hali ya kuanza mazungumzo."

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Africa Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Africa Moussa Faki Mahamat

Guterres anasema amekua akiwasiliana na pande zote katika juhudi za kusitisha mapigano na kusema kwamba yeye na mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Africa Moussa Faki Mahamat wanakubaliana juu ya yale yanayobidi kufanyika.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Billene Seyoum hakujibu maswali ya waandishi wa habari hii leo juu ya matamshi ya Guterres wala mpango wa Marekani wa kutafuta njia za kuzuia mapigano.

XS
SM
MD
LG