Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:42

Ethiopia: Abiy ataka raia kujiunga katika vita vya Tigray dhidi ya TPLF


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Serikali ya Ethiopia imewataka raia wake kujiunga katika mapigano yanayoendelea kati yake na vikosi vya wapiganaji  wa Tigray, ambavyo, inasema, sasa vimeendeleza mapigano hata nje ya eneo lake, katika vita vya miezi tisa, ambavyo vimepelekea kuwepo kwa mzozo mkubwa wa wakimbizi.

Wito huo wa kutaka raia kujihami umetolewa kupitia taarifa ya afisi ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambayo ilieleza kuwa “huu ni wakati mwafaka kwa Waethiopia wote wenye uwezo, walio na umri wa kujiunga na vikosi vya ulinzi na vikosi maalum, kuonyesha uzalendo wenu.”

Taarifa hiyo imejiri wiki sita baada ya serikali ya Ethiopia, peke yake, kutangaza kusitishwa kwa mapigano katika jimbo la kaskazini mwa nchi, la Tigray, katika siku ambapo wapiganaji wa chama cha TPLF, walichukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle. Ethiopia ilitangaza hatua hiyo baada ya miezi minane ya mapigano.

Vita vilizuka mwezi Novemba mwaka jana kati ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na vikosi vya TPLF, chama ambacho kilitawala Ethiopia kwa miongo mitatu, na sasa kinadhibiti jimbo la Tigray. Mapigano hayo yamelazimisha zaidi ya watu milioni mbili kuhama makwao, na zaidi ya watu 50,000 wamekimbilia katika nchi jirani ya Sudan.

Taarifa hiyo, ambayo imepuuzwa na vikosi vya Tigray, haikutaja kusitisha mapigano, na viongozi wa TPLF wamesema serikali ya Ethiopia inapaswa kukubaliana na masharti yake kwa amani.

Wasemaji wa vikosi vya Tigray na wa waziri mkuu Abiy hawakupatikana mara moja kutoa kauli zaidi kwa shirika la hanabari la Tigray.

Baada ya kuchukua tena udhibiti wa Tigray mwishoni mwa Juni na mapema Julai, vikosi vya Tigray vimeingia katika maeneo ya karibu ya Afar na Amhara.

"Mapigano hayo mapya yamewahamisha zaidi ya watu 250,000 katika Afar na Amhara," mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa alisema wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG