Kama sehemu ya ripoti mpya, Amnesty ilizungumza na manusura 63 wa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kutoka Tigray, pamoja na wataalamu wa afya wanao wahudumia manusura.
Kati ya manusura, 38 walisema ubakaji huo ulifanywa na wanajeshi wa Eritrea.
Waathirika waliwekwa kizuizini kwa zaidi ya saa 24, na wakati mwingine kwa wiki kadhaa huku wakibakwa na wanajeshi, alisema Fisseha Tekle, mtafiti wa Amnesty International kwa Pembe ya Afrika alipozungumza na AP.
Ethiopia na Eritrea wote wameilaumu ripoti hiyo.