Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:59

Eliud Kipchoge achukua dhahabu tena olimpiki

 Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kuvunja rekodi ya marathon alipokuwa Vienna.
Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kuvunja rekodi ya marathon alipokuwa Vienna.

Eliud Kipchoge ameibuka tena kuwa mshindi wa mbio za Marathon Japan akichukua tena medali ya dhahabu baada ya kukimbia kwa muda wa saa mbili dakika 8 na sekunde 38.

Eliud Kipchoge ameibuka tena kuwa mshindi wa mbio za Marathon Japan akichukua tena medali ya dhahabu baada ya kukimbia kwa muda wa saa mbili dakika 8 na sekunde 38.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 36 alimaliza kwa zaidi ya sekunde 80 mbele ya mshindi wa pili Abdi Nageeye wa Uholanzi. Naye Bashir Abdi wa Ubelgiji alipata medali ya shaba. Kipchoge alitabasamu njiani na hata kumsalimu kwa ngumi mwanariadha mwenzake. Kipchoge anaweka historia ya kuwa mwanariadha wa tatu kushinda medali nyingi za dhahabu katika mbio za wanaume, akijiunga na Abebe Bikila (1960, '64) na Waldemar Cierpinski ('76, '80).

Kipchoge, akiwa amevalia raba za Nike nyeupe-na-pinki na aliwaacha wenzake katika kiasi cha kilomita 30 mpaka karibu na kumaliza hakukuwa na mtu hata wa karibu. Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu alishika nafasi ya 7 akitumia muda wa saa mbili dakika 11 na sekunde 35 nao wanariadha kadhaa walishindwa kumaliza akiwamo Ken Kipruto wa Kenya na Gerald Gabriel wa Tanzania na Stephen Kiprotich wa Uganda akiwamo pia Lelisa Desisa wa Ethiopia.

XS
SM
MD
LG