Maafisa wa jimbo hilo Jumatatu wameripoti kwamba zaidi ya watu 200, wakiwemo watoto 100 waliuawa katika shambulio hilo ambalo wanasema lilitokea siku ya ijumaa.
Vyanzo vimeiambia Nation Africa kwamba tukio hilo lilitokea baada ya makombora ya mizinga kurushwa kwenye kambi ya waliolazimishwa kuhama makazi yao inayopatikana wilaya ya Galicoma.
Hata hivyo, mkuu wa mawasiliano katika jimbo hilo, Ahmed Haloita ameiambia BBC kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na wapiganaji washirika wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF). Maafisa wa TPLF hawakupatikana ili kutoa maelezo juu ya madai hayo.
Kufuatia habari za mauaji hayo ya kutisha, shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) limeelezea wasiwasi wake wakati likitoa wito kwa pande zote kufanya kila liwezekanalo, ili kulinda watoto dhidi ya madhara.
“Kuongezeka kwa mapigano huko Afar na maeneo mengine jirani ya Tigray, ni kitu kibaya kwa watoto”, taarifa iliyotolewa na mkuu wa UNICEF Henrieta Fore imesema.