"Ethiopia itaimarisha hali yake ikiwa itazingatia kile Sudan inaweza kufanya .. badala ya kukataa kabisa juhudi zake zote," ilisema taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Sudsan.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatano juu ya mzozo katika jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia, ambao umesababisha kuwepo kwa wakimbizi wapatao 53,400 tangu mwishoni mwa mwaka 2020.
Ombi la Hamdok la kutaka kuwa mpatanishi limejiri wakati wa muhula wake kama mwenyekiti wa IGAD, kikundi cha kieneo, ambacho kinajumuisha Kenya, Ethiopia, Uganda, Djibouti, Sudan, Sudan Kusini, Uganda na Somalia, ilisema taarifa hiyo.