Ombi la Hamdok la kutaka kuwa mpatanishi limejiri wakati wa muhula wake kama mwenyekiti wa IGAD, kikundi cha kieneo, ambacho kinajumuisha nchi nane.
Serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita imesema inafanya kazi na taasisi za kimataifa kama vile FAO kuelekea katika kuongeza ujuzi kwa wakulima kukabiliana na kiangazi kwa kufufua kilimo cha umwagiliaji.
Msemaji wa WFP Bettina Luescher amesema yapata watu milioni 800 duniani ambao wanakabiliwa na njaa.
Shirika la WFP kupitia akaunti yake ya Twitter limesema mchango huo mpya wa Marekani “ umekuja wakati mwafaka ambao tayari familia nyingi kipindi hiki cha mwaka zimeishiwa kabisa akiba zao za vyakula.”
Mchumi wa kilimo Paul Makube, ambaye anafanya kazi na First National Bank ya Afrika Kusini, ameiambia VOA inaleta tija kuzungumzia kuhusu kilimo wakati panapo zungumziwa kujenga masoko yenye ushindani, na kuboresha ubunifu na teknolojia.
Tatizo la ukame barani Afrika, viboko waangamia kisiwani Lamu, Kenya
Tatizo hilo tayari limezikumba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusababisha uhaba wa chakula kwa baadhi ya wananchi na pia kuendelea kuwepo kwa mfumuko wa bei za mazao ya nafaka.
Seylici amesema “Sisi tunaikaribia njaa, tathmini tuliofanya na ile iliofanywa na mashirika ya misaada inaonyesha njaa iko karibu kutangazwa upande wa mashariki ya eneo la Somaliland,
Shirika la wakimbizi la UN linaripoti kuwa wananchi wa Sudan Kusini milioni 1.6 wamekimbilia nchi jirani kutokana na njaa, vita na ukame, wakiifanya Sudan Kusini kuwa na tatizo la wakimbizi linalo ongezeka kwa kasi duniani.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watoto 50,000 katika eneo la Somaliland na Somalia wanakabiliwa na balaa la kupoteza maisha kwa sababu ya ukame unaoendelea katika eneo hilo.
Kufuatia upungufu wa mvua, Rais Kenyatta amesema ukame umeendelea kuathiri zaidi ya Wakenya milioni mbili kutoka kaunti zaidi ya kumi na mbili. Pia kuna ripoti kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka na kuongeza baa la njaa.
Pandisha zaidi