Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:13

FAO yaeleza changamoto za kilimo kusini mwa Afrika


Zao la mahindi lililoharibiwa na ukame Kusini mwa Afrika
Zao la mahindi lililoharibiwa na ukame Kusini mwa Afrika

Idara ya Umoja wa Mataifa ya chakula na Kilimo (FAO) inasema vipindi virefu vya kiangazi, mvua chache, viwango vya juu vya joto na kuwepo kwa janga la viwavi jeshi, mambo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliharibu msimu wa upandaji kusini mwa afrika mwaka 2018 na kuvuruga matarajio ya uvunaji binafsi.

Katika mahojiano na mratibu wa FAO kwa eneo la kusini mwa Afrika, Chimimba David Phiri, amesema kutokana na sababu hizo msimu wa uzalihsaji nafaka mwaka 2018 umeathiriwa vibaya ukilinganisha na msimo wa mwaka 2016 / 2017 ambapo eneo hilo lilishuhudia mvua za kawaida.

“Katika misingi ya uzalishaji chakula kusini mwa Afrika, wasi wasi ni kwamba mwaka huu mvua zimechelewa kunyesha, na hata kama zitakuja, huenda zisinyeshe kama inavyotarajiwa ukichanganya na kipindi kirefu cha kiangazi katika ya msimu. Kwahiyo nadhani, tutakuwa na matokeo yasiyo mazuri katika uzalishaji wa jumla mwaka huu,” amesema Phiri.

Katika baadhi ya maeneo, ikiwemo Zimbabwe, viwavi jeshi, ambao mara ya kwanza walionekana msimu uliopita, ukichanganya na hali inavyoendelea kusambaa amesema Phiri, wadudu hao msimu huu wako kote katika eneo la SADC isipokuwa Mauritius na Lesotho.

Lakini kwa mkulima Moses Juliis Chibaya, kiasi cha kilometa 200 kaskazini mwa Harare, viwavi hivyo vikilenga mazao ya mahindi. Anasema angeweza kuvuna idadi nzuri ya tumbaku kama ilivyokuwa mwaka jana kama isingekuwa kwa kipindi cha kiangazo ambacho Zimbabwe inakabiliana nacho.

Chibaya anasema, “ingawaje uchumi wetu haufanyi vizuri, lakini kwa mtizamo wa mkulima wa kawaida, nadhani tunahitaji kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji na serikali lazima isadia katika kutoa vifaa. Na pengine kama wataweza kuwapa mikopo wakulima.”

Mwaka 2000, serikali ya Rais wa zamani Robert Mugabe ilipitisha mpango wa mageuzi ya ardhi ambao iliwaondoa wakulima wengi wazungu kutoka kwenye mashamba yao na kuwapatia wakulima weusi ardhi hiyo. Hatua hiyo ilisababisha uharibifu katika maeneo mengi yenye kilimo cha umwagiliaji ambacho kilitumiwa sana na wakulima wa biashara na hiyo ikasababisha kushuka kwa uzalishaji kilimo nchini Zimbabwe.

Serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita imesema inafanya kazi na taasisi za kimataifa kama vile FAO kuelekea katika kuongeza ujuzi kwa wakulima kukabiliana na kiangazi kwa kufufua kilimo cha umwagiliaji.

XS
SM
MD
LG