Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:55

Ramaphosa achaguliwa rais mpya Afrika Kusini


Rais Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa

Bunge la Afrika Kusini limemchagua rasmi Cyril Ramaphosa kama rais mpya wa nchi hiyo Alhamisi.

Ramaphosa alichaguliwa bila ya kupigiwa kura baada ya kuwa ndiye mgombea pekee aliyeteuliwa katika bunge mjini Cape Town, Jaji Mkuu Mogoeng Mogoeng aliwaambia wabunge.

Baada ya jaji mkuu kutangaza hilo wabunge wa chama cha ANC waliibuka kuimba na kucheza wakishangilia.

Kuchaguliwa kwa Ramaphosa kumekuja masaa kadhaa baada ya Jacob Zuma kujiuzulu “mara moja”baada ya viongozi wa chama tawala cha ANC kuamua aachie madaraka mapema wiki hii, wakiwa wamechoshwa na miaka yake tisa ya uongozi iliyokuwa imegubikwa na madai ya ufisadi na kudidimia kwa uchumi.

Hata hivyo Ramaphosa anakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kuendeleza uchumi ambao ulikuwa umedidimia. Sarafu ya rand, ya Afrika Kusini leo imefikia kiwango kizuri katika soko la fedha dhidi ya dola ya Marekani katika kipindi cha miaka mitatu kufuatia kujiuzulu kwa Zuma.

Ramaphosa, ambaye alikuwa makamu wa rais chini ya utawala wa Zuma, alikuwa tayari ni mrithi wa Zuma baada ya kuchaguliwa kama rais wa ANC mwezi Disemba 2017.

XS
SM
MD
LG