Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:23

Vijana wa Ethiopia waombwa kujiunga kwenye mapigano dhidi ya Tigray


Kifaru kilichoharibiwa kwenye mapigano ya Tigray
Kifaru kilichoharibiwa kwenye mapigano ya Tigray

Jimbo la Ethiopia la Amhara Jumapili limetoa wito kwa vijana wote kuchukua silaha dhidi ya wapiganaji wa Tigray ambao wanapambana na jeshi la serekali kuu pamoja na wanajeshi wa majimbo mengine tisa.

Wito huo wa hamasa kubwa dhidi ya wapiganaji wa Tigray’s People Liberation Front ,TPLF ambao jeshi la Amhara limesema wanalishambulia sasa , wameendelea na vita vya zamani vya miezi nane na vurugu katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

“Ninatoa wito kwa vijana wote, wanamgambo na wasiokuwa wanamgambo, kuchukua silaha yoyote ya serekali, kuchukua silaha zao binafsi, na kujiunga na operesheni ya vita dhidi ya TPLF kuanzia Jumatatu”, rais wa serekali ya jimbo la Amhara Agegnehu Teshager, amenukuliwa na chombo cha habari cha serekali akisema hayo katika jimbo hilo.

Vita vilizuka mwezi Novemba kati ya jeshi la Ethiopia na chama cha TPLF ambacho kinaongoza jimbo hilo la kaskazini mwa nchi. Wiki tatu baadaye, serekali ilitangaza ushindi ilipoteka mji mkuu wa Tigray, Mekelle, lakini TPLF waliendelea kupigana. Mwishoni mwa mwezi Juni, TPLF walidhibiti Mekelle na eneo kubwa la Tigray baada ya wanajeshi wa serekali kuondoka.

XS
SM
MD
LG