Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 17:14

Sudan yamtaarifu balozi wa Ethiopia kuokotwa maiti 29 za raia wake


Ramani ya Ethiopia ikionyesha eneo la Tigray na Sudan
Ramani ya Ethiopia ikionyesha eneo la Tigray na Sudan

Sudan imemwita balozi wa Ethiopia huko Khartoum kumjulisha kuwa maiti 29 zilizopatikana kwenye kingo za mto katika mpaka na Ethiopia ni za raia wa Ethiopia.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imeongeza kuwa miili hiyo ni ya watu kutoka kabila la Tigray.

Taarifa hiyo iliyotolewa Jumanne jioni imeeleza kwamba balozi huyo aliitwa Agosti 30 na alijulishwa kwamba miili hiyo ilipatikana kati ya Julai 26 na Agosti 8.

Miili hiyo iliokotwa upande wa Sudan wa Mto Setit, unaojulikana nchini Ethiopia kama Tekeze.

Maiti hizo zilitambuliwa na Waethiopia wanaoishi katika eneo la Wad al Hulaywah mashariki mwa Sudan, taarifa ilisema.

Taarifa hiyo haikusema jinsi watu hao walivyokufa.

Dina Mufti, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia, hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

XS
SM
MD
LG