Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:47
VOA Direct Packages

Wakimbizi wafarijika kwa kuwezeshwa kukutana na kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving Marekani


Wakimbizi wafarijika kwa kuwezeshwa kukutana na kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving Marekani
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00

Wakimbizi kutoka kote duniani ambao wako eneo la Washington watakutana pamoja kusherehekea sikukuu ya kwanza ya kutoa shukrani, yaani Thanksgiving, nchini Marekani.

Katika nchi mpya waliyopokelewa, Marekani, mamia ya wakimbizi kutoka sehemu zote duniani walikusanyika mapema mwezi Novemba kusherehekea Thanksgiving. Hawa wakimbizi walisherehehekea kwa mara ya kwanza sikukuu hii. Anila Karimzai, Mkimbizi wa Afghanistan anaeleza: “Kwa kuja hapa, najihisi vizuri na nina furaha kuwa na kila mtu, kuna watu wengine kutoka sehemu mbali mbali. Nina furaha kushiriki katika sherehe za Thanksgiving na watu wengi wanafuraha.” Thanksgiving nchini Marekani inaadhimishwa kila mwaka katika Alhamisi ya nne ya mwezi Novemba.

Makundi

XS
SM
MD
LG