Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:17

Marekani yaishutumu vikali Afghanistan kwa kuzuia elimu kutolewa kwa wanawake


FILE - Picha ya Oct. 13, 2022, Wanafunzi wa kike wa Afghanistan wakipanga mstari kuingia kufanya mtihani katika Chuo Kikuu cha Kabul.
FILE - Picha ya Oct. 13, 2022, Wanafunzi wa kike wa Afghanistan wakipanga mstari kuingia kufanya mtihani katika Chuo Kikuu cha Kabul.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeushutumu vikali uongozi wa Taliban baada ya serikali ya Afghanistan kupiga marufuku wanawake kusoma katika vyuo vikuu binafsi na vya umma nchini Afghanistan.

Ni amri ya karibuni ya kuzima haki za wanawake na uhuru na hatua hiyo inaanza mara moja.

Uamuzi huo ulitangazwa baada ya mkutano na serikali ya Taliban.

Licha ya ahadi za awali kuwa watakuwa na kanuni za wastani na wataheshimu haki wanawake na haki za walio wachache, Taliban kwa kiasi kikubwa imetekeleza tafsiri yao kali ya sheria za kiislamu.

Wamewapiga marufuku wasichana kutokwenda shule kuanzia shule za kati mpaka za sekondari, na kuwawekea masharti wanawake kuanzia katika ajira na kuwaamuru kujifunika kuanzia kidogo gumba cha mguu hadi kichwani wakiwa hadharani.

Wanawake pia wamepigwa marufuku kwenda kwenye bustani na maeneo ya mazoezi.

Barua ambayo imetolewa na msemaji wa wizara ya elimu ya juu, Ziaullah Hashmi imesema vyuo vikuu binafsi na vya umma vinatakiwa kutekelza marufuku hiyo haraka iwezekanavyo na kuijulisha wizaara yake mara marufuku hiyo inapotekelezwa.

XS
SM
MD
LG