Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 10:40

Afghanistan: Wanafunzi 16 wauawa katika shambulio la bomu


Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, Abdul Nafi Takoor katika mkutano na waandishi wa habari , mjini Kabul, Juni 8, 2022. Picha ya Reuters
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, Abdul Nafi Takoor katika mkutano na waandishi wa habari , mjini Kabul, Juni 8, 2022. Picha ya Reuters

Maafisa nchini Afghanistan leo Jumatano wamesema wanafunzi 16 wameuawa na wengine 27 kujeruhiwa wakati bomu liliporipua shule ya kidini au madrasa, kaskazini mwa mkoa wa Samangan.

Afisa anayehusika na habari Imdadullah Mahajer, ameithibitishia VOA vifo hivyo kwa njia ya simu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani mjini Kabul, Abdul Nafi Takoor, amesema shambulio hilo la bomu katika mji mkuu wa mkoa, Aybak, lilitokea wakati wanafunzi wakifanya sala ya alasiri.

Takoor amesema maafisa wa usalama na ujasusi wa Taliban walifika eneo la tukio kufanya uchunguzi na watafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulio hilo, hata hivyo kundi la Islamic State katika mkoa wa Khorsan au ISIS-K linashukiwa kwa shambulio hilo, ni tawi la Islamic State nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG