Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:15

Siku ya Wakimbizi Duniani : UNHCR yakiri wakimbizi wakabiliwa na ubaguzi, shutuma, uadui


Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi
Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi

Leo ni siku ya wakimbizi duniani. Wakati ulimwengu ukiwa unakabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutokana na migogoro inayoendelea kutokea katika nchi mbalimbali.

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi ameeleza bado kunaudhaifu katika kushughulikia idadi kubwa ya wakimbizi.

Grandi amekiri kwamba kile kinachomtatiza ni hali hii ya mazingira ya wakimbizi iliyo na ubaguzi, shutuma na inayowaona wakimbizi, wahamiaji na wakati mwingine raia wa kigeni kuwa maadui. Ni mtazamo ambao wengi wanazingatia kwa sababu ya hofu, lakini haipaswi kuwa hivyo..

Amesema licha ya hali hiyo ya watu wengi kupoteza makazi yao kwa sababu ya kukimbia vita,migogoro na ukandamizaji wa haki za binadamu bado inaweza kushughulikiwa . Alitolea mfano ufanisi wa Uganda ambayo imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Grandi amesema kuwa Uganda haina raslimali zote kwa hivyo ukarimu huo haupaswi kupuuzwa na kwamba inapaswa kusaidiwa. Aliongeza kuwa kwa kuiga mfano huo ambao kwasasa unatekelezwa katika takriban mataifa 15, kuna muongozo mpya kwa kusaidia kwa njia bora zaidi mzozo huo wa wakimbizi.

Ameongeza kuwa shirika la UNHCR limefichua kwamba idadi kubwa ya watu walilazimika kuyakimbia makazi yao mwaka 2018 kwa sababu ya vita, unyanyasaji na migogoro. Shirika la UNHCR lilitoa takwimu Jumatano zinazoonyesha katika kipindi cha mwaka 2018, watu takriban milioni 71 walipoteza makazi yao.

Kwa mujibu wa idhaa ya habari ya Ujerumani, DW, kabla ya siku ya kimataifa ya wakimbizi, Kamishna huyo alisema, kumekuwa na udhaifu mkubwa katika kushughulikia idadi kubwa ya wakimbizi.

Aliongeza kuwa wametambua kuwa bara la Ulaya kwa mfano limejipanga kwa idadi ndogo tu ya wakimbizi na kwamba idadi ya wakimbizi ilipoongezeka mwaka 2015, bara hilo halikuwa limejiandaa na wimbi hilo na hivyo kutuma ujumbe usiofaa.

Grandi aliwashtumu baadhi ya wanasiasa ambao wametumia hali hiyo vibaya na kwamba wametambua kuwa kwa kuwaonyesha watu hawa kuwa tishio watapata uungwaji mkono na kura. Aliongeza kuwa hii ni mbinu isiyostahili ya kulishughulikia suala hili na haitatui tatizo lililoko.

XS
SM
MD
LG