Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:01

UNHCR : Idadi ya wakimbizi milioni 71 ni ya juu kufikiwa kwa miaka 70


Wakimbizi wa Somalia wakisubiri kusafirishwa kwenda Kismayo, Somalia, chini ya programu ya kuamua bila shuruti kurejea nchini kwao, kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya, Disemba 19, 2017.
Wakimbizi wa Somalia wakisubiri kusafirishwa kwenda Kismayo, Somalia, chini ya programu ya kuamua bila shuruti kurejea nchini kwao, kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya, Disemba 19, 2017.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaripoti kuwa watu milioni 71 duniani wamelazimika kuhama makazi yao kwa sababu ya vita, unyanyasaji na migogoro, ikiwa ni idadi ya juu kabisa ya wikimbizi kufikiwa tangu UNHCR kuundwa miaka 70 iliyopita.

Shirika hilo linaiita idadi hiyo ya milioni 70.8 ni ya siku za nyuma kwa sababu mgogoro wa Venezuela haukujumuishwa. Shirika hilo linakadiria kuwa takriban wananchi wa Venezuela milioni 4 wamekimbia nchi yao, lakini wengi wao hawajaomba hifadhi ya ukimbizi rasmi, ikiwafanya wasiweze kuhisabiwa na wakimbizi wengine.

Mwaka 2018, ripoti hiyo inasema, vita na migogoro viliwalazimisha takriban watu milioni 26, nusu yao watoto, kukimbia nchi zao. Zaidi ya watu milioni 41 walilazimika kukimbia makazi yao ndani ya nchi, wakikimbia majumba yao lakini bado wakiishi ndani ya mataifa yao.

Ripoti hiyo imesema zaidi ya thuluthi mbili za wakimbizi wote duniani wanatokea nchi tano tu – Sudan Kusini, Syria, Afghanistan, Somalia, na Myanmar.

Kwa mwaka wa tano mfululizo, Uturuki ilipokea idadi ya juu kabisa ya wakimbizi, ikifuatiwa na Uganda, Sudan, Pakistan, na Ujerumani.

Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Wakimbizi Filippo Grandi amesema takwimu zinaonyesha kuwa nchi tajiri duniani hawabebi mzigo mkubwa kabisa wa wakimbizi.

“Unaposema kuwa nchi za Ulaya zinampango wa dharura wa wakimbizi au Marekani au Australia – Hapana,” Grandi amesema.

“Wengi kati ya hao wakimbizi ukweli ni kuwa wako katika nchi zilizoko jirani na vita na, bahati mbaya, inamaana nyingi katika nchi hizo ni maskini au zenye vipato vya kati. Na ndiko migogoro ilipo. Na huko ndipo tunatakiwa tuaangaze.”

Grandi ameiambia VOA nchi za Kiafrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara zinaendelea kuwa ni zenye migogoro ya zamani, inayojirudia na mipya. “Old – ni mfano wa Somalia. Inayojirudia au kutokea mara kwa mara – kwa mafano Burundi au DRC, Sudan Kusini, inayojirudia zaidi kuliko nchi zote. Migogoro mipya – mfano wa hali ya baadhi ya maeneo yanayo zungumza Kiingereza Cameroon. Hali hii kwa namna fulani ni mpya. Kuna wakimbizi 30,000 kutoka Cameroon huko Nigeria na kuna idadi kubwa ya wananchi Cameroon walilazimika kuhama makazi yao nchini mwao.

Grandi anasisitiza kuwa wakimbizi wanataka kurudi makwao. Kwa bahati mbaya, wanalazimika kuishi katika hali isifahamika hatma yake kwa vipindi virefu kwa sababu hatua ya kupata suluhisho la tatizo lao inaendelea kuwa ni ngumu.

Amesema kuwa vita vipya ambavyo vinasababisha wakimbizi wengi zaidi zinazuka haraka zaidi kuliko vile suluhisho la migogoro hiyo inavyoweza kupatikana kwa watu ambao wamelazimika kuhama makazi yao.

Kati ya watu zaidi ya milioni 70 ambao walilazimika kuhama makazi yao mwaka 2018, ripoti ya UNHCR inasema chini kidogo ya wakimbizi 600,000 waliweza kurejea nchini mwao, na wengine 92,400 tu waliweza kupelekwa kuishi nchi nyingine.

XS
SM
MD
LG