Mashua mbili zilipatikana zikiwa katika bahari ya Mediterranean kati ya nchi ya Morocco na Algeria na Rasi ya Liberia huku zikiwa na watu 80, kumi na tatu kati yao wakiwa wamepoteza maisha.
Walinzi wa Spain pia wameokota maiti nne na kuokoa watu wengine 22 kwenye pwani ya bahari ya Atlantic kusini mwa mji wa Cadiz.
Spain sasa imekuwa kituo kikuu cha wahamiaji wanaovuka kinyume cha sheria na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati ambayo wanajaribu kuingia Ulaya.
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) linalo simamia wahamiaji linasema zaidi ya watu elfu 47 wamejaribu kuvuka kwenda Spain kati ya Januari 1 na Oktoba 30, 2018.