Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:57

Baraza la UN limepiga kura kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi


Wakimbizi kutoka baadhi ya mataifa duniani wakisubiri msaada
Wakimbizi kutoka baadhi ya mataifa duniani wakisubiri msaada

Marekani na Hungary yalikuwa mataifa mawili pekee ambayo yalipiga kura dhidi ya Global Compact on Refugees wakati mataifa 181 yalipiga kura ya kukubaliana na suala hilo

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lilipiga kura Jumatatu kupitisha muundo wa kuimarisha majibu ya kimataifa ya mgogoro wa wakimbizi duniani.

Marekani na Hungary yalikuwa mataifa mawili pekee ambayo yalipiga kura dhidi ya Global Compact on Refugees wakati mataifa 181 yalipiga kura ya kukubaliana na suala hilo. Eritrea, Libya na Jamhuri ya Dominican hawakupiga kura.

Amina Mohammed, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Amina Mohammed, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed katika kukaribisha kura hiyo alisema “Ni jukumu la ulimwengu kuchukua hatua na kubeba majukumu yetu kuhusu wakimbizi, kutafuta masuluhisho ambayo yanaheshimu haki zao za binadamu, kuwapatia matumaini na kutambua wajibu wa kisheria wa kuwalinda na kuwasaidia. Amina aliwasihi wanachama wote kuanza kuutekeleza muundo huo haraka iwezekanavyo.

​
XS
SM
MD
LG