Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Wakimbizi wa Rohingya wanavyokabiliwa na maambukizo


Wakimbizi wa Rohingya wakisubiri msaada wa chakula katika kambi ya wakimbizi Bangladesh
Wakimbizi wa Rohingya wakisubiri msaada wa chakula katika kambi ya wakimbizi Bangladesh

Maji machafu na msongamano wa vibanda na hali ya uchafu imetengeneza mazingira muwafaka kwa kuenea maradhi ambayo yanaweza kuzuiliwa katika kambi ya wakimbizi ya Balukhali Bangladesh.

Kambi hiyo iko eneo la Cox’s Bazaar, mji ulioko kusini mashariki mwa Bangladesh. Ni makazi kwa Waislamu wa Rohingya takriban 650,000 waliokimbia machafuko katika nchi jirani ya Myanmar.

Zaidi ya vikundi 200 vinavyozunguka tayari vimeshatoa dozi 900,000 za kinga ya ugonjwa wa kolera kwa wakimbizi. Lakini, tayari maambukizo mengine ya vijidudu vyenye maambukizo, vijulikanavyo kama diphtheria, vimejitokeza.

“Diphetheria ni ugonjwa ambao unaweza kuepukwa kwa dawa za kinga,” amesema Kate Nolan ambaye anafanya kazi na kikundi cha kimataifa cha misaada cha Madaktari wajulikanao kama madaktari bila mipaka.

Nolan ameongeza kusema kuwa inaelekea kuwa maambukizi ya diphtheria yanaonyesha watu wa Rohingya hawakuwa na huduma nzuri ya afya walipokuwa nchini Myanmar, ambayo pia inajulikana kama Burma.

Maradhi ya diphtheria aghlabu yanasababisha utando mweupe wenye kugandana kukusanyika katika pua na koo.Maambukizo hayo huathiri kupumua na kuuathiri moyo na mfumo wa fahamu katika mwili wa mwandamu. Bila ya kupata matibabu, diphtheria husababisha kifo.

XS
SM
MD
LG