Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:31

Ukosefu wa damu Uganda wasababisha vifo kwenye hospitali kadhaa


Wagonjwa katika hospitali moja ya Uganda.
Wagonjwa katika hospitali moja ya Uganda.

Upungufu wa damu katika hospitali kadhaa nchini Uganda umepelekea maafa katika baadhi ya vituo na taasisi za afya katika maeneo mbalimbali.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, visa vya wanawake wajawazito kupoteza maisha yao kutokana na ukosefu wa damu vimeripotiwa kwenye hospitali za Kawempe na Arua, huku baadhi ya wagonjwa wakihamishiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mulago, ili kupokea matibabu ya dharura.

Mkurugenzi wa hospitali ya Mulago, Dkt Evelyn Nabunya, alithibitisha vifo hivyo lakini hakutoa idadi kamili ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na hali hiyo.

Msemaji wa hospitali hiyo, Enock Kusasira, amenukuliwa na gazeti hilo akisema kuwa kuna upungufu wa aina mbalimbali za damu yani blood groups.

Kufuatia hayo, huduma ya damu nchini Uganda imezindua kampeni ya utoaji damu, ili kukabiliana na hali hiyo.

XS
SM
MD
LG