Waziri wa mambo ya nje wa Colombia - Carlos Holmes Trujillo- amesema kwamba idadi ya wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini Colombia kutoka Venezuela, huenda ikaongezeka marudufu na kufikia watu milioni 4 ifikapo mwaka 2021 iwapo hali ya mgogoro ya Venezuela haitapata suluhu la haraka.
Zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia Venezuela katika miaka ya hivi karibuni wakitafuta chakula na dawa katika nchi jirani, huku hali ya kisiasa na uchumi ya Venezuela ikiendelea kuwa mbaya Zaidi.
Takriban raia milioni moja wa Venezuela wanaishi katika nchi jirani ya Colombia.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na chama chake cha kisosholisti wamefutilia mbali idadi ya raia wan chi hiyo wanaotorokeea nchi jirani kama wakimbizi akidai kwamba idadi inayotolewa vita cya kisiasa.