Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:04

UN, wapiganiaji haki watahadharisha urejeo wa wakimbizi wa Rohingya


Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters Wa Lone akitoka mahakamani akishikiliwa na polisi huko Yangon, Myanmar Aprili 11, 2018.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters Wa Lone akitoka mahakamani akishikiliwa na polisi huko Yangon, Myanmar Aprili 11, 2018.

Serikali ya Myanmar Jumamosi imesema imeanza kuwapokea familia ya kwanza ya wakimbizi wa kabila la Rohingya nchini humo.

Makundi ya kupigania haki za binadamu yamesema kuwa hatua hiyo ni kitendo cha kutafuta njia ya kujisafisha kwa serikali hiyo kwani mpaka hivi sasa kuna hali ya wasiwasi kwa kukosekana usalama kwa wakimbizi wa Rohingyas wanaorejea ambalo bado halijapatiwa ufumbuzi.

Kikundi kinacho washughulikia wakimbizi cha Umoja wa Mataifa (UN) wamesema Ijumaa kuwa hali ya usalama nchini Myanmar bado hairidhishi kwa wakimbizi hao kuwa salama, kuheshimiwa na kuweza kujikimu kimaisha.

Jukumu la kuhakikisha hali hiyo inafikiwa ni la serikali ya Myanmar na hili lazima lisiishie tu kutayarisha makazi, mahitaji muhimu na miundo mbinu.

Serikali ya Myanmar imesema katika tamko lake kuwa familia tano zimekamilisha taratibu za kurejea nchini humo na hivi sasa wanaishi kwa muda na ndugu zao katika mji wa Maungdaw, karibu na mpakani, kati ya Myanmar na Bangladesh.

Tamko hilo limesema kuwa familia hiyo imepata tayari kitambulisho cha uthibitisho cha taifa. Lakini kitambulisho hicho hakiwatambulishi watu hao kama raia wa Myanmar.

Viongozi wa Rohingya wamevikataa vitambulisho hivyo, wakisema kuwa wanataka haki kamili za uraia wa watu wa Rohingyas ambao wamekabiliwa na ukandamizaji na mateso huko Myanmar kwa miongo mingi.

XS
SM
MD
LG