Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:23

Hisia juu ya shambulizi la Marekani, Uingereza, Ufaransa dhidi ya Syria


Wanajeshi wa Syria wakishangilia na kutoa matamko dhidi ya Rais Trump baada ya shambulizi la anga lililofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Wanajeshi wa Syria wakishangilia na kutoa matamko dhidi ya Rais Trump baada ya shambulizi la anga lililofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Hisia mbalimbali zimejitokeza duniani ikiwa baadhi ya watu wanaunga mkono mashambulizi hayo na wengine kukosoa shambulizi hilo la anga lililofanywa mapema Jumamosi na majeshi ya Marekani, Ufaransa na Uingereza dhidi ya vituo vya serikali ya Syria.

Ndege za kivita za nchi za Ulaya na manuari za kijeshi zilishambulia kwa makombora vituo vitatu vya silaha za kemikali nchini Syria, shambulizi la awali ambalo linaweza kugeuka kuwa ni muendelezo wa kampeni ya kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al- Assad na wanao muunga mkono.

Katika mkutano wa waandishi wa habari London Jumamosi, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema nia ya kuratibu mashambulizi haya sio kwa ajili ya “kuipindua serikali,” lakini ni “kupunguza na kuzuia” uwezo wa serikali ya Assad kutumia silaha za kemikali.

Ameongeza kuwa jumuiya ya kimataifa haiwezi kusimama kando na “kutupia macho tu” wakati utawala wa Syria ukiendelea kutumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake.

Huko Paris, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa tamko akisema, “ Hatuwezi kuvumilia kitendo cha kufanya matumizi ya silaha za nyuklia ni mwenendo wa kawaida,” akiongeza kuwa “ukweli wa taarifa na kuhusika kwa utawala wa Syria hauna mashaka.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anaunga mkono mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza.

Amesema mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa yanapaswa kuwa onyo kwa utawala wa Syria kutoendelea kutumia silaha za sumu.

Wakati huohuo Serikali ya Iran imesema imesema kuwa Marekani, Ufaransa na Uingereza hazitaweza kupata manufaa yoyote kwa kuishambulia Syria.

Mamia ya wananchi wa Syria walijitokeza katika mji mkuu wa Damascus, Jumamosi wakiendesha magari huku honi zikilia, wakionyesha alama ya ushindi na kupeperusha bendera za Syria kwa kupinga mashambulizi ya kijeshi ya pamoja yaliyofanywa na nchi hizo tatu. Wengine walikuwa wakipiga makelele wakisema, "Sisi ni watu wako, Bashar."

Washirika wa Syria, ikiwemo Russia wamesema kuwa shambulizi hilo la pamoja dhidi ya Syria limefeli. Wizara ya mambo ya nje imesema idadi kubwa ya makombora yaliyopigwa Syria yaliangamizwa na mfumo ya ulinzi wa serikali ya Syria.

XS
SM
MD
LG