Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:06

Kenya :Maafisa wa serikali wafunguliwa mashtaka ya ufisadi


Kampeni dhidi ya ufisadi nchini Kenya: wananchi waandamana kupinga vitendo vya ufisadi.
Kampeni dhidi ya ufisadi nchini Kenya: wananchi waandamana kupinga vitendo vya ufisadi.

Mahakama nchini Kenya Jumatatu imewafungulia mashtaka maafisa wa ngazi ya juu kutoka shirika la bomba la mafuta linaloendeshwa na serikali na wengine kutoka Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa kwa kutumia vibaya madaraka na uhalifu wa kiuchumi iliyo sababisha mabilioni ya fedha kupotea katika taasisi hizo mbili.

Dazeni ya maafisa wa serikali ya Kenya na wafanyabiashara walianza kufikishwa mahakamani tangu mwezi Mei wakituhumiwa na makosa yanayo husiana na madai ya kuhusika na wizi wa mamia ya bilioni za shilingi kutoka katika akaunti za umma, ikiwa ni hatua mpya ya kupambana na ufisadi.

Joe Sang, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bomba la mafuta la Kenya, na wenzake watano wamefunguliwa mashtaka wakituhumiwa kutumia vibaya madaraka yao kesi hiyo ikihusishwa na upotevu wa fedha katika ujenzi wa kituo cha kushushia mafuta magharibi mwa Kenya yenye thamani ya shilingi bilioni 1.96 ($19 milioni), kiwango ambacho kimevuka bajeti ya awali iliyokuwa imepangwa kutumika.

Geoffrey Mwangi, Afisa mtendaji mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, mrithi wake katika ofisi hiyo na maafisa wengine 16 wamefunguliwa mashtaka ya kutumia madaraka yao vibaya, kupokea zawadi zisizo kubalika na kuongeza muda wa mkataba ambapo shilingi bilioni 1.1 zilipotea.

Washtakiwa wote walikanusha makosa waliokuwa wanatuhumiwa nayo.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameahidi kupambana na ufisadi wakati alipochaguliwa kuwa rais mwaka 2013, lakini wakosoaji wa serikali yake wanasema amekuwa akisuasua kuwafuatilia maafisa wa ngazi ya juu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya rushwa. Tangu achukue madaraka hakuna mtu wa ngazi ya juu aliyewahi kuhukumiwa kwa vitendo vya ufisadi.

XS
SM
MD
LG