Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:55

Naibu wa jaji mkuu Kenya akamatwa kwa shutuma za ufisadi


Jaji Philemona Mwilu. Naibu wa jaji mkuu wa Kenya.
Jaji Philemona Mwilu. Naibu wa jaji mkuu wa Kenya.

Naibu wa jaji mkuu wa Kenya, Philemona Mwilu, alikamatwa mjini Nairobi Jumanne kwa shutuma za ufisadi.

Baada ya kukamatwa na maafisa wa upelelezi, Jaji Mwilu alipelekwa hadi kwa makao makuu ya idara ya upelelezi ili kuhojiwa kufuatia tuhuma kwamba amekuwa akihusika na visa vya ulaji rushwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji na mkuu wa idara ya upelelezi, George Kinoti, walihudhuria mikutano kadhaa na maafisa wa tume ya huduma ya mahakama kabla ya kukamatwa kwa Mwilu.

Baadaye, Haji aliitisha kikao na wanahabari.

Gazeti hilo limesema kwamba mamlaka ya forodha ya Kenya iliripoti kwa idara mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kuwa jaji huio alikwepa kulipa kodi ya kiasi kikubwa cha fedha na alihusika katika uadhirifu wa pesa kupitia benki mbalimbali.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa afisa wa ngazi za juu wa kiwango hicho kutiwa mbaroni kwa shutuma za ufisadi.

Jumatatu, vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba jaji mmoja alikuwa akitafutwa na maafisa wa upelelezi kwa shutuma za ulaji rushwa.

Habari zaidi zitafuata...

XS
SM
MD
LG