Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:45

Wizi NYS Kenya: Washtakiwa 24 wanyimwa dhamana


Watu wakiandamana kulaani vitendo vya ufisadi mjini Nairobi, Kenya Feb 17, 2010.
Watu wakiandamana kulaani vitendo vya ufisadi mjini Nairobi, Kenya Feb 17, 2010.

Washtakiwa 24 wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za Shirika la Vijana la Huduma ya Taifa (NYS) watawekwa rumande kwa kipindi cha wiki moja.

Jaji ameamrisha washukiwa hao wakae ndani na uamuzi wa kuachiliwa kwa dhamana utafanyika Jumatatu wiki ijayo.

Kati ya walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai, vyanzo vya habari vimeripoti Jumatano.

Mapema Jumatatu wiki hii vyombo vya usalama nchini Kenya vilimtia nguvuni Ndubai ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa wizi wa takriban Dola za Marekani milioni 100, vyombo vya habari vimeripoti Jumatatu, na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai alisema watu 17 walikuwa wanashikiliwa na polisi.

Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao Kenya wameipongeza serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kwa hatua iliyochukua dhidi ya ufisadi.

Katika tamko la pamoja ikiwemo Marekani na Uingereza, wameeleza kuwa watakaopatikana na hatia wachukuliwe hatua, ikiwemo kutaifishwa mali yao inayotokana na ufisadi.

XS
SM
MD
LG