Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:39

Washukiwa wa kesi ya Olympiki wafikishwa mahakamani Kenya


Aliyekuwa waziri wa michezo wa Kenya, Hassan Wario.
Aliyekuwa waziri wa michezo wa Kenya, Hassan Wario.

Katibu Mkuu wa zamani wa wizara ya michezo, Utamaduni na Sanaa nchini Kenya, Richard Titus Ekai, ni miongoni mwa watu waliofikishwa mbele ya  hakimu mkuu mjini Nairobi Jumatatu, kwa tuhuma za ufisadi, katika sakata iliyogonga vichwa vya habari wakati wa mashindano ya olimpiki ya mwaka wa 2016,  mjini Rio de Janeiro, Brazil, mwaka 2016.

Pamoja na Ekai, wengine waliofunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa ni afisa mkuu aliyeongoza ujumbe wa wanariadha wa Kenya kwa mashindanio hayo ya Olimpiki, Stephen Soi, na Katibu mkuu wa kamati ya kitauifs ys Oli,mpiki nchini Kenya, Francis Paul Kinyili.

Kufuatia kukamatwa kwa maafisa hao mwishoni mwa wiki, walifikishwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama inayosikiliza kesi za ufisadi, iliyo eneo la Milimani katika jiji kuu la Kenya, Nairobi.

Pamoja na ufisadi, watatu hao pia walishtakiwa kwa shutuma za matumizi mabaya ya mamlaka.

Baadhi ya maafisa hao wanakabiliwa na madai ya kutaifisha pesa za wakimbiaji walioshinda medali mjini Rio.

Pesa hizo hutoka kwa kampuni ya Marekani ya kutengeza vifaa ya michezo Nike ambayo hutoa $15,000 kwa mshindi wa dhahabu, $7,500 kwa mshindi wa fedha na $5000 kwa wanaopata medali ya shaba.

Maafisa hao watatu wameachiliwa kwa dhamana ya shilinggi milioni moja sawa na dola10,000 za Kimarekani, na kuaguizwa kupeana hati zao za usafiri kwa polisi

Wakati huo huo, aliyekuwa waziri wa michezo, Utamaduni na Sanaa, wa Kenya, HASSAN Wario, amepewa hadi Jumatano asubuhi, kujiwasilisha mkwa idara ya upelelezi, na baadaye kufika mahakamani siku ya Ijumaa.

Wahiga Mwaura, mwanahabari wa shirika la habario la Royal Media Services, ambaye aliandamana na timu ya Kenya hadi Rio De Jenairo na kuripoti kuhusu sakata hii kwa kirefu, alizungumza na VOA akiwa mjini London Uingereza.

"Nilihisi dosari kadhaa zilizopelekea uamuzi wangu kwamba kulikuwa na kkashfa kubwa kuliko ilivyoonekana kwa wakati huo," alisema Mwaura.

Wario, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Kenya nchini Austria, ni miongoni mwa maafisa saba wanaochunguzwa upya na idara ya upelelezi kuhusu madai ya ufujaji wa $872,867 sawa na 88,000,000 za Kenya katika michezo hiyo ya Olimpiki.

Aidha aliyekuwa rais wa kamati ya kitaifa ya olimpiki na bingwa wa zamani wa mbio za Olimpiki, Kipchoge Keino, pamoja na maafisa wengine wawili, walitakiwa kujiwasilisha kama waziri huyo wa zamani.

Ripoti ya kamati ya kuchunguza kashfa hiyo inaeleza kwamba pesa hizo zilikua ni za tiketi za ndege za kikosi cha Kenya lakini maafisa walipandisha bei ya tiketi hizo kupita kiasi kwa manufaa yao wenyewe.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuewa na malalamiko baina ya mabingwa wa riadha wa Kenya, kwamba wanaoshinda medali katika michezo ya Olimpiki na ya Jumuiya ya Madola wamekua hawapewi pesa hizo kutoka kwa wafadhili kama kampuni ya Nike.

XS
SM
MD
LG