Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:10

Uswizi kusaidia Kenya kurejesha fedha zilizoporwa - Rais


Marais Uhuru Kenyatta na Alain Berset kwenye mkutano kati ya ujumbe wa Usizi na ule wa Kenya katika ikulu ya Nairobi.
Marais Uhuru Kenyatta na Alain Berset kwenye mkutano kati ya ujumbe wa Usizi na ule wa Kenya katika ikulu ya Nairobi.

Rais wa Uswizi, Alain Berset, namwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Jumatatu walitia saini makubaliano mbalimbali, ikiwa ni pama na yale ya ushirikiano katika vita dhidi ya ufisadi.

Berset anaendelea na ziara ya siku mbili nchini Kenya, wakati rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta, kwa mara nyingine tena akiahidi kuimarisha juhudi zake za kukabiliana na ufisadi ambao umekuwa kero kubwa kwa miaka mingi.

Viongozi hao waliingia makubaliano kwamba serikali ya Uswizi itarejesha fedha zinazofungamana na uhalifu na ufisadi na ambazo zinaendelea kuhifadhiwa katika benki za taifa hilo la ulaya.

Wawili hao aidha walikubaliana kwamba Kenya itafungua ubalozi mpya katika jiji kuu la nchi hiyo, Bern.

Hii hapa ripoti ya mwandishi wa Sauti ya Amerika, Kennedy Wandera akiwa Nairobi:

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00

XS
SM
MD
LG