Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:44

Majaji wala rushwa wadaiwa kudumaza juhudi za Kenyatta


Jengo la mahakama Kenya
Jengo la mahakama Kenya

Majaji wala rushwa wanazuia mapambano dhidi ya rushwa nchini Kenya, na kudumaza juhudi za rais Uhuru Kenyatta kurejesha uaminifu wa umma katika serikali, usalama wa taifa na uchumi, mwendesha mashtaka wa juu nchini amesema.

Kila mwaka, rushwa katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki inachukua mabilioni ya dola kutoka kwenye mifuko ya serikali kwa njama zinazohusisha maafisa wa serikali na wafanyabiashara, kwa kile kinacho julikana kama ‘tenda za ujasiriamali’ kwa kuweza kupata kandarasi za umma.

Kenyatta aliahidi kusitisha uozo wa ufisadi wakati alipoingia madarakani mwaka 2013, lakini wakosoaji wanasema ana kwenda pole pole kuwafuatilia maafisa wa juu na hakuna kesi zinazo wahusu maafisa wa juu tangu wakati huo.

Mwendesha mashtaka mpya wa umma, Noordin Mohammed Haji, naibu mkuu wa zamani wa upelelezi wa taifa, anajaribu kubadili hilo, na wiki hii alimshtaki gavana mmoja wa kaunti kwa mara ya kwanza kwa kosa la rushwa.

Hivyo hivyo, mwezi Mei mamlaka iliwashtaki zaidi ya watu 50 wengi wao wafanyakazi wa serikali, wakihusishwa na wizi wa takriban $ milioni 100 ya fedha za umma kutoka taasisi ya Taifa ya Huduma za Vijana (NYS), idara ya serikali. Usikilizaji wa awali wa kisheria unaendelea katika kesi hiyo.

Haji, ambaye alichukua madaraka mwezi Machi, amesema mapungufu katika mfumo wa sheria, ni pamoja na majaji na waendesha mashtaka kuweza kuhongwa, jambo ambalo linaweza kuvuruga hata kesi zenye ushahidi wa kutosha.

“Kama una maafisa wa mahakama ambao wamekumbwa na hali hiyo na kutoa maamuzi dhidi ya yako, hoja itakuwa kesi ilikuwa dhaifu,” aliliambia shirika la habari la Reuters, na kuelezea kwamba moja ya waendesha mashtaka wake alikamatwa mwezi uliopita kwa shutuma za rushwa. “Hatuwezi kutia vichwa vyetu kwenye mchanga,” amesema.

Msemaji wa mahakama hakuweza kupatikana haraka kujibu shutuma za Haji. Msemaji wa rais Kenyatta pia hakupatikana kutoa maoni yake.

Uhaba wa wafanyakazi na malipo duni ni tatizo jingine. Kenya ina waendesha mshtaka wa umma 500 katika taifa lenye watu milioni 45, na mwendesha mashtaka wa chini analipwa kiasi cha $ 600 kwa mwezi, Haji amesema, ukilinganisha na wabunge ambao wanalipwa kiasi cha $10,000.

“Nina mawakili wachache tu ambao wanaweza kuendesha kesi za rushwa,” amesema.

Baada ya miaka 19 katika idara ya upelelezi, Haji amesema ameonga kwa macho yake mwenyewe jinsi rushwa inavyoingilia usalama wa Kenya, kwa mfano, wanamgambo kutoka nchi jirani ya Somalia wanavuka mpaka kwa hati za kusafiria ambazo wamezipata kwa njia ya rushwa.

Rushwa pia imegharimu maisha ya watu kwa kupitia urasimu amesema.

Wiki hii, Haji amewashtaki wafanyabiashara tisa na maafisa kwa mashtaka ya kuua bila ya kukusudia kwa kuhusika na ujenzi wa bwawa kinyume cha sheria ambalo lilikuwa kwenye shamba moja la maua, bwawa hilo lilipasuka na kuua takriban watu 50.

Kenya ina sheria ya kuzuia majanga kama hayo, Haji amesema, ‘lakini kwasababu ya rushwa hilo lilipuuzwa.’

XS
SM
MD
LG