Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:31

Marekani kuisaidia Kenya kupambana na rushwa


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akizungumza na ujumbe kutoka Matrekani wakati wa mkutanio wa uwekezaji uliofanyika kwenye makao ya Umoja wa Mataifa, mjini Gigiri, Nairobi, Kenya. Juni 28, 2018.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akizungumza na ujumbe kutoka Matrekani wakati wa mkutanio wa uwekezaji uliofanyika kwenye makao ya Umoja wa Mataifa, mjini Gigiri, Nairobi, Kenya. Juni 28, 2018.

Marekani imesema iko tayari kuisaidia Kenya katika vita dhidi ya ufisadi. Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec, Alhamisi alimwambia rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwamba utawala wa Trump una matumaini kwamba janga hilo litakabilianwa nalo vilivyo ili kuimarisha mazingira ya uwekezaji.

Godec alikuwa akizungumza mjini Nairobi wakati wa mkutano wa uwekezaji ambao uliongozwa na naibu wa waziri wa masuala ya biashara za kimataifa, Gilbert Kaplan, na uliohudhuriwa na ujumbe wa takriban wafanyabiashara 60 kutoka Marekani.

Kenyatta aliwaambia wawekezaji kutoka Marekani kwamba utawala wake utawahakikishia mazingira mema ya kufanya biashara, na kwamba hatalegeza kamba katika vita dhidi ya ulaji rushwa kwenye serikali yake.

Kwa mara ya kwanza, Kenyatta alizumgumzia shutuma kwamba kakake mdogo, Muhoho Kenyatta, huenda anahusika katika sakata ya uingizaji wa sukari nchini, ambayo inashukiwa kuwa na viwango vya juu vya kemikali hatari kwa afya ya binadamu.

Rais huyo aidha alisema ana imani na vyombo vya dola vinavyofanya uchunguzi na kuongeza kwamba iwapo ndugu yake anashukiwa kuhusika katika kashfa hiyo, basi na afunguliwe mashtaka kama Wakenya wengine.

"Hakuna haja ya kuingiza siasa katika suala hili. Iwapo ndugu yangu anashukiwa, basi na ashtakiwe kama wengine," alisema Kenyatta.

Katika siku za karibuni Kenyatta ameonyesha ukakamavu katika juhudi za kupamabana na ulaji rushwa kwenye idara za serikali.

Hata hivyo, wakaosoaji wake wanamshutumu kwamba huenda watu walio karibu naye wasishtakiwe wala kufungwa, hata kama watapatikana na hatia ya kuhusika kwenye kashfa za ufisadi na visa vingine vya kuvunja sheria.

Ujumbe huo wa Marekani uko kwenye ziara ya siku tatu nchini Kenya, na unajumuisha baraza la kumshauri rais wa Marekani kuhusu biashara barani Afrika.

Makubalianao kadhaa ya kibiashara ilitiwa saini wakati wa hafla hiyo.

XS
SM
MD
LG