Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 18:11

Historia ya Maisha ya Marehemu Jimmy Carter

Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter ambaye alihudumu kwa muhula mmoja tu madarakani kutoka 1977 mpaka 1981, katika kipindi cha urais ambacho kilikuwa na changamoto za uchumi na mzozo wa matekani nchini Iran.

Wakati alipoondoka White House baada ya kushindwa kuchaguliwa tena, Carter alirejea nyumbani kwake Plains, Georgia, bila ya wazo la wazi ni kipi kitakachofuata. Wakati wa enzi yake ya urais inakumbukwa zaidi kwa matatizo kuliko mafanikio, Carter alikuwa mmoja war ais wa zamani ambaye alifanikisha mengi katika historia ya Marekani, alianzisha Carter Center shirika ambalo si la kiserikali mwaka 1982, na kwa zaidi ya miongo minne alitetea demokrasia, haki za binadamu na afya ya umma kote duniani.


Makundi

XS
SM
MD
LG