Kit Burns, mkazi wa jimbo la Washington katika mji wa Tacoma, anamkumbuka vizuri Carter kwa kazi yake ya kujenga nyumba kwa watu wenye uhitaji.
Naye Kit Burns, Mkazi wa Jimbo la Washington anaeleza kuwa: "Kuna idadi kubwa ya nyumba za Habitat for Humanity karibu na ninapoishi. kujitolea kwake kuliwasaidia watu wengine, nadhani hilo ndiyo lengo kuu kwa sisi sote katika maisha yetu. Ni jambo lisilofaa wakati wengine wakitaabika hatutoi msaada na tunao uwezo wa kufanya hivyo. amekuwa mfano wa kuigwa kwa miaka mingi."
Carter alionyesha umuhimu wa kuwajali watu, anasema Natosha Walker, mkazi wa Virginia. Anasema kuwa: Katika utumishi wa umma, upo hapa kuwahudumia watu. Hiyo ndiyo sifa muhimu sana. Na kuongoza kwa mfano. Alikuwa anafundisha mafunzo ya Biblia. Alikuw ana Habitat for Humanity. Hiyo ni mifano mizuri ya jinsi tunavyopaswa kuongoza, tunavyopaswa kushirikiana na Wa-marekani wenzetu.
Wakati huo huo Soko la Hisa la New York lilikaa kimya kwa dakika kadhaa, kutoa heshima kwa rais huyo wa zamani kabla ya kupiga kengele yake ya ufunguzi hapo Jumatatu.
Mkazi wa New Jersey, Delores Spivak anakumbuka kazi za Carter kwa Wa-israeli na Wa-palestina.
Spivak anaeleza kuwa: "Mimi nina wasiwasi sana juu yake. Ninaogopa urais wake, kwa sababu yeye ndiye aliyepigania mazingira, haki za kiraia. Lakini baadaye, vitabu vyake alivyoandika, hasa kuhusu Mashariki ya Kati, vilikuwa vikubwa. Mwili unatetemeka ninapozungumza, ninapofikiria juu ya makubaliano ya Camp David."
Kifo cha Carter ni fursa ya kujifunza zaidi kuhusu maisha yake na urais, anasema mkazi wa Connecticut, Kim Potvin.
Potvin anasema kuwa: "Nafikiria sana sera zake ambazo alijihusisha nazo ambazo sikuwa nazifahamu, na pia uchumi na historia ya wakati huo. Kila wakati nadhani tunajifunza mengi kutoka kwenye historia kwa sababu inatafsiri masuala mengi yanayoendelea leo."
Katika mji wa Plains anakoishi Carter, kwenye jimbo la Georgia. Sandra Walters anamkumbuka rafiki ambaye walikua nae mtaani.
Walters, ambaye ni rafiki wa Carter alikuwa na haya ya kusema: "Asante Mungu kwa kumpatia Maisha ya miaka mia moja, na kufanya mambo yote ambayo alitaka kuyafanya. Nadhani alitimiza mengi sana, hakuna mtu atakayekuwa na huzuni juu ya mtu yeyote ambaye alifanya kila mtu huyo alikifanya, kutoka mji mdogo huko Plains, Georgia, alilelewa kwenye shamba la karanga na akawa rais wa Marekani."
Carter atazikwa katika mji wa Plains, baada ya mazishi ya kitaifa mjini Washington hapo Januari 9.
Forum