Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:44

Ethiopia yaripotiwa kufunga mitandao ya kijamii


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Ethiopia imezuia mitandao ya kijamii Facebook, Whatsapp na Instagram, taasisi inayofuatilia matumizi ya mitandao ya kijamii, Netblocks imesema Jumatatu.

Mkurugenzi wa Netblocks Alp Toker ameliambiia shirika la habari la Reuters kwamba mitandao hiyo ya kijamii imezuiliwa katika maeneo sita nchini Ethiopia.

Mitandao ya kijamii kama Twitter, Youtube, Snapchat, LinkedIn na Reddit bado inafanya kazi, Toker amesema.

Wanaotumia mitandao ya kijamii wenye huduma za VPN wanaweza kufanya kazi licha ya mitandao hiyo kuzuiliwa, Toker ameongeza.

Jumamosi, tume ya uchaguzi nchini Ethiopia ilisema uchaguzi wa bunge uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 5 Juni umeahirishwa hadi tarehe nyingine ambayo haijatangazwa kutokana na changamoto za kiufundi.

Huduma ya internet ilizuiliwa miaka ya nyuma wakati wa mizozo ya kisiasa, huduma hiyo ilifungwa mwaka 2020 katika jimbo la kaskazini la Tigray baada ya jeshi la Ethiopia kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa TPLF baada ya ngome zake kushambuliwa.

XS
SM
MD
LG