Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:30

UN yasema matukio 500 ya ubakaji yameripotiwa Tigray


Wakimbizi waliokimbia vita jimbo la Tigray wakiwasili kwenye eneo la Mto Tekeze katika mpaka wa Sudan-Ethiopia, Hamdayet, mashariki ya Sudan. (AP Photo/Nariman El-Mofty, File)
Wakimbizi waliokimbia vita jimbo la Tigray wakiwasili kwenye eneo la Mto Tekeze katika mpaka wa Sudan-Ethiopia, Hamdayet, mashariki ya Sudan. (AP Photo/Nariman El-Mofty, File)

Umoja wa Mataifa umesema Alhamisi kuwa zaidi ya visa 500 vya ubakaji vimeripotiwa kwenye vituo vitano ya afya kwenye eneo la Ethiopia la Tigray.

Pia inasema huenda idadi ikawa kubwa zaidi kutokana na baadhi ya waathirika kutoripoti pamoja na ukosefu wa huduma za afya.

Wakati akihutubia kikao cha UN mjini New York, naibu mratibu wa misaada nchini Ethiopia, Waafa Said amesema kuwa wanawake wamedai kubakwa na watu waliokuwa na silaha,

Waathirika hao wamesema wamebakwa na makundi ya watu na kubakwa mbele ya familia zao pamoja na wanaume kulazimishwa kubaka watu wa familia zao baada ya kutishiwa maisha yao.

Said ameendelea kusema kuwa takriban visa 516 vya ubakaji vimeripotiwa kwenye vituo vitano vya afya kwenye miji ya Mekelle, Adigrat, Wukro, Shire na Axum.

Kundi la maafisa wa Umoja wa Mataifa mapema wiki hii limetoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi na ukatili wa kingono dhidi ya raiya kwenye eneo la Tigray.

Mjumbe maalum wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Taye Atske Selassie Amde amesema kuwa serikali yake inachukulia madai hayo kwa uzito mkubwa na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea kufanywa.

XS
SM
MD
LG