Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:25

Ripoti ya Marekani yadhihirisha mauaji ya kutokomeza kabila moja Tigray


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na Kulia ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Abi Ahmed.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na Kulia ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Abi Ahmed.

Ripoti ya ndani ya serikali ya Marekani ambayo gazeti la The New York Times imeipata inasema kuwa Ethiopia inaendesha “kampeni maalum ya kutokomeza kabila moja”.

Kampeni hiyo inafanyika kwa kisingizio cha vita katika mkoa wa Tigray, eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linadhibitiwa na wanamgambo wa Amhara upande wa kaskazini mwa nchi.

Gazeti la The Times linaeleza kuwa ripoti hiyo, iliyoandikwa mapema Februari, inafafanua “waziwazi ardhi inayoshuhudia nyumba zilizovamiwa na kuibiwa thamani zake na vijiji vilivyotelekezwa ambapo maelfu ya watu hawajulikani walipo.”

Kulingana na gazeti la Times ripoti hiyo imegundua kuwa maafisa wa Ethiopia na wapiganaji ambao ni washirika wao kutoka mkoa jirani wa Amhara, ambao wlaihamia Tigray kumsaidia Waziri Mkuu Abiy Ahmed, wanafanya “kwa makusudi na ufanisi mpango wa kuhamisha kabila mmoja la Tigray Magharibi kwa kutumia nguvu na manyanyaso.”

Ramani ya Axum, Ethiopia.
Ramani ya Axum, Ethiopia.

Ripoti hiyo inasema baadhi ya watu walikimbia msituni au walivuka mpaka kinyume cha sheria kuingia Sudan, na wengine walizingirwa na kulazimishwa kuhamia maeneo mengine ya Tigray, kulingana na gazeti hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema katika taarifa yake Jumamosi kuwa Marekani “ina wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za ukatili na hali kwa ujumla inavyoendelea kuwa mbaya huko Tigray.

Marekani “imerejea mara kadhaa kuwasiliana na serikali ya Ethiopia juu ya umuhimu wa kumaliza ghasia, na kuhakikisha misaada ya kibinadamu haizuiliwi kufika Tigray, na kuruhusu uchunguzi kamili wa kimataifa ulio huru kufuatia ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu, manyanyaso, na mauaji,” Blinken amesema, akiongeza kwamba wale waliohusika na vitendo hivyo “lazima wawajibishwe.”

Blinken ameutaka Umoja wa Afrika, na washirika wa kieneo na kimataifa kufanya kazi na Marekani kutatua mgogoro wa Tigray, ikiwemo hatua kupitia UN na vyombo vengine husika.

Blinken pia alieleza harakati za wanajeshi wa Eritrea huko Tigray.

“Hatua ya mara moja ya kuondoa vikosi vya Eritrea na vikosi vya eneo vya Amhara kutoka Tigray ni hatua za kwanza muhimu” Blinken amesema.

“Hatua hizo zifuatiwe na tamko la pamoja la kusitisha mapigano na pande zote husika katika mgogoro huo na ahadi ya kuruhusu misaada kuwafikia wale walioko Tigray.

Kiongozi wa Warepublikan kwenye Kamati ya Mambo ya Nje katika Baraza la Wawakilishi, Michael McCaul, pia ametoa taarifa Jumamosi, akiusihi utawala wa Biden “kuchukua hatua kuwawajibisha wale waliohusika na mauaji ya aina yoyote “ katika mkoa wa Tigray.

“Hili lazima lipewe kipaumbele cha juu wakati Marekani ikichukua jukumu la Uwenyekiti wa Baraza la Usalama mwezi ujao,” amesema McCaul.

Vita vya Tigray vimeua maelfu ya watu. Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kufuatia vita hiyo. Eneo hilo lenye zaidi ya watu milioni 5 linakabiliwa na upungufu wa chakula, maji na dawa.

XS
SM
MD
LG