Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:24

Burundi na Ethiopia zakubaliana kuimarisha ushirikiano


Rais President Evariste Ndayishimiye (Photo by TCHANDROU NITANGA
Rais President Evariste Ndayishimiye (Photo by TCHANDROU NITANGA

Rais Sahle Work Zewde wa Ethiopia akamilisha ziara ya siku mbili nchini Burundi ambako alikuwa na mazungumzo na Rais Everiste Ndayishimiye juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

Mazungumzo yao yaligusia ushirikiano wa kikanda na viongozi hao wameongelea pia suala la kuboresha matumizi ya maji ya mto wa Nile ili kuepusha mizozo inayojiri mara kwa mara kwenye mto huo.

Kabla ya kuhitimisha siku ya Jumatano hii ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Burundi, Rais wa Jamhuri ya Ethiopia alilakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye na kufanya tathmini kwa undani zaidi juu ya jitihada maridhawa za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo ni ushahidi thabiti wa uhusiano mwema kati ya mataifa ya Burundi na Ethiopia, Rais amethibitisha kwenye ikulu yake katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura.

Wakati huo huo, Rais Ndayishimiye amesema kwamba : "Majadiliano hayo yaligubikwa hasa hasa na utashi wa kila upande wa kuinua sekta ya uwekezaji na ubadilishanaji wa biashara kati ya mataifa hayo mawili."

Ikizingatiwa kuwa Burundi na Ethiopia ni miongoni mwa nchi zinazotumia maji ya mto Nile, Rais wa Jamhuri ya Ethiopia amesisitiza kwa upande wake kuhusu umuhimu wa usatawi wa mto huo, akihakikisha kwamba : "Ni zawadi waliokabidhiwa na Mwenyezi Mungu na ni kitovu kinachounganisha nchi mbali mbali, kwa hiyo maji ya mto wa Nile yanastahili kutumiwa katika hali ya amani kwa faida ya wote."

Marais hao wawili wamechukua fursa hiyo na kubadilishana maoni kuhusu suala la mzozo unaozikabili nchi za Ethiopia na Misri kuhusu matumizi ya maji ya mto wa Nile, kufuatia mradi wa nchi ya Ethiopia wa ujenzi wa bwawa kubwa la umeme kwenye mto huo.

Imearifiwa pia kwamba Rais wa Ethiopia amemshawishi Rais wa Burundi kuunga mkono nchi ya Ethiopia katika mzozo huo, ikimaanisha kuwa mtangulizi wake Hayati Rais Pierre Nkurunziza alikuwa na msimamo wa kuunga mkono taifa la Misri.

Itafahamika kwamba ziara hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Ethiopia ni ya kwanza ya rais wa nchi hiyo nchini Burundi tokea Rais Ndayishimiye achaguliwe kutawala taifa la Burundi mwezi wa Juni mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG