Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 09:55

Burundi: Waandishi habari 4 waachiliwa huru na Rais Ndayishimiye


Waandishi wa habari 4 wa Burundi walioachiliwa huru Alhamisi Disemba 24 na Rais Evariste Ndayishimiye.
Waandishi wa habari 4 wa Burundi walioachiliwa huru Alhamisi Disemba 24 na Rais Evariste Ndayishimiye.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye Alhamisi aliwasahemehe wanahabari wanne wa jarida la mtandaoni Iwacu, ambao walikua wanazuiliwa jela tangu Oktoba mwaka wa 2019.

Wanahabari hao Agnes Ndirubusa , Christine Kamikazi, Egide Harerimana na Terence Mpozenzi walihukumiwa na mahakama ya mwanzo na ile ya rufaa kifungo cha miaka 2 na nusu jela kwa shutuma za kuhatarisha usalama wa taifa, wakati walikua wamekwenda kuchunguza habari kuhusu mapigano kati ya kundi la waasi na wanajeshi wa serekali katika mkoa wa magharibi wa Bubanza.

Baadaye walikata rufaa kwenye mahakama ya juu ya Burundi.

Mkurugenzi wa jarida la Iwacu Antoine Kaburahe, ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter, “walihukumiwa miaka miwili na nusu jela kwa madai yasiokua na msingi. Walimuomba rais awasamehe, na sasa tunapongeza kuachiliwa kwao."

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, washington DC.

XS
SM
MD
LG