Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:46

Jeshi la Ethiopia ladai kuuwa wana TPLF


ETHIOPIA-TIGRAY-CONFLICT-UNREST
ETHIOPIA-TIGRAY-CONFLICT-UNREST

Jeshi la Ethiopia limesema Jumapili kuwa limeuwa wanachama 15 kutoka chama cha Tigray People’s Liberation Front, TPLF, huku wengine wanane wakikamatwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, brigedia jenerali kutoka jeshi la serikali amekiambia chombo cha habari cha serikali kwamba miongoni mwa watu waliokamatwa ni aliekuwa kiongozi wa Tigray, Abay Weldu huku miongoni mwa waliouwawa wakiwa ni pamoja na aliekuwa naibu mkuu wa polisi wa eneo.

Serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed alitangaza ushindi dhidi ya TPLF kwenye eneo la Tigray hapo Novemba 28, baada ya karibu mwezi mmoja wa mapigano. Hata hivyo viongozi wa TPLF wameapa kuwa wataendelea na mapambano wakati wakiwa kwenye milima ingawa Reuters hawajaweza kuwafikia kwa wiki kadhaa sasa.

Wakati huo huo ripoti zinasema kuwa mazungumzo kati ya Ethiopia, Sudan na Misri kuhusiana na bwawa kubwa la uzalishaji umeme la Ethiopia yamekwama, mataifa yote matatu yamesema Jumapili. Hata hivyo kupitia taarifa tofauti, Misri na Ethiopia wanalaumu hatua ya Sudan ya kukataa mkakati mpya wa mazungumzo.

Mazungumzo kuhusu bwawa hilo lililogharimu dola bilioni 4 yamekuwa yakiendelea hata baada ya kuanza kujazwa maji mwezi Julai mwaka uliopita.

Imetayarishwa na Harrison Kamau.

XS
SM
MD
LG