Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:05

Mazungumzo kuhusu bwawa la Ethiopia kwenye mto Nile kuanza tena


Bwawa la Ethiopia - Grand Renaissance
Bwawa la Ethiopia - Grand Renaissance

Sudan, Egypt na Ethiopia, zimekubaliana kufanya mazungumzo zaidi mwezi huu katika jaribio jingine la kusuluhisha mgogoro wa mda mrefu kuhusu bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Ethiopia kwenye mto Blue Nile.

Mazungumzo ya awali kuhusu bwawa hilo yalikosa kufikia makubaliano kuhusu kiasi ambacho Ethiopia inastahili kujaza maji bwawa la Grand Renaissance

Maswala yenye utata yanahusu namna Ethiopia inastahili kujaza maji bwawa hilo kila mwaka iwapo msimu wa ukame unatokea na namna nchi hizo zinastahili kutatua migogoro inayoweza kujitokeza katika siku zijazo.

Ethiopia imekataa pendekezo la kusitisha mradi wake wakati upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa kiasi cha asilimia 97 hasa kwa shughuli za kilimo na maji ya kunywa, ina wasiwasi kwamba bwawa la Ethiopia litapunguza kiwango cha maji.

Sudan, ambayo ilisusia mazungumzo ya mwezi Novemba ikitaka umoja wa Afrika kuingilia kati na kuhakikisha makubaliano yanapatikana, ina matumaini kwamba bwawa hilo litasaidia kuzuia mafuriko, lakini imeonya kwamba maisha ya mamilioni ya watu huenda ikawa katika hatari iwapo hakuna mkataba maalum utafikiwa.

Ethiopia imesema kwamba umeme utakaozalishwa na bwawa hilo ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wake, na inasisitiza kwamba halitatatiza kwa namba yoyote kiwango cha maji kwenye mto huo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG