Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:18

Marekani yaitaka Ethiopia iruhusu uchunguzi wa mauaji Tigray ufanyike


Waziri wa Mambo ya Nje Marekani Anthony Blinken (Kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri wa Mambo ya Nje Marekani Anthony Blinken (Kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaeleza ghasia za karibuni katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia ni juhudi za kuangamiza kabila moja akitoa wito uchunguzi ufanyike na majeshi ya Eritrea yaondoke mara moja.

Mwana diplomasia huyo wa juu wa Marekani alisema hayo alikua wakati anaeleza vipaumbele vya sera za kigeni vya utawala mpya mbele ya kamati ya masuala ya kigeni ya Baraza la Wawakilishi la bunge Jumatano.

Antony Blinken alizungumzia masuala mbali mbali ya kigeni na namna wanavopanga kukabiliana na mizozo inayoendelea duniani kwa wakati huu. Akiulizwa juu ya mzozo wa kibinadamu katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia, Blinken alilaani vikali kile alichokieleza ni vitendo vya kuangamiza watu wa Tigray na kukomeshwa ukiukaji wa haki za binadam katika jimbo hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema : "Waziri mkuu Abiy alikuwa kiongozi mwenye mwenye kuleta matumaini aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel. Hivi sasa inabidi aiimarishe juhudi zake ili kuhakikisha raia wake wa Tigray wanapata usalama wanaohitaji na wanaostahili kupewa.

Blinken anasema amekua akizungumza kwa simu mara kadhaa na Waziri Mkuu Abiy na viongozi wengine wa kanda hiyo kujaribu kutafuta njia za kumaliza ghasia dhidi ya raia.

Berhan (siyo jina lake halisi )miaka 30, asili yake Edaga Hamus, akiwa hospitali Mekele, on Februari 27, 2021. - inadaiwa alibakwa na kundi la wanajeshi wa Eritrea and Ethiopia katika matukio matatu tofauti.
Berhan (siyo jina lake halisi )miaka 30, asili yake Edaga Hamus, akiwa hospitali Mekele, on Februari 27, 2021. - inadaiwa alibakwa na kundi la wanajeshi wa Eritrea and Ethiopia katika matukio matatu tofauti.

Blinken kadhalika aliieleza kamati hiyo kwamba atakutana na wanadplomasia wa juu wa China wiki ijayo na kujadli masuala kadhaa yanao tia wasiwasi Marekani.

Alisema atakutana Kwanza na waziri mwenzake huko Alaska akiwa njiani anarudi kutoka ziara ya Japan na Korea Kusini. Tangazo hlo liliwasababisha wabunge kumuuliza masuala mengi ambayo aliwahakikishia atajadili kwa kina na wenyeji wake, na kusema hii itakua ni mkutano wa Kwanza tu.

Blinken amefafanua : "Hakuna nia kwa wakati huu kuandaa mfululizo ya mikutano. Ikiwa kutakua na haja ya kuendeleza mazungumza itategemea mapendekezo yanayotokana na maendeleo ya kweli kuhusiana na mambo yanayozusha wasi wasi kati yetu na China.

Blinken alikubaliana pia na wabunge wengi wa vyama vyote viwili kwamba ukandamizaji unaofanywa na China dhdi ya wa Waislamu wa kabila la Uighur na watu wa makabila ya waliowachache katika jimbo la Xinjiang inafikia kiwango cha mauaji ya kimbari na akatoa wito kwa Bejing kuruhusu jumuia ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuingia katika jimbo hilo. Akisema Ikiwa hawana la kuficha basi tuonyesheni yanayotokea huko.

Warepublican kadhaa waliulza suala la wahamiaji wanao jaribu kuingia kwa wingi Marekani kupitia mpaka wake wa kusini na Mexico. Mbunge Mrepublican Michael Mccaul alimuliza kwa nini utawala wa Biden ulifuta makubaliano yaliyotiwa saini kati ya utawala wa Trump na mataifa ya Amerika ya Kati.

McCaul ameeleza :Tunashuhudia ongezeko kubwa la wahamiaji wanaovuka na kusababisha mzozo mkubwa kwenye mpaka wetu wa kusini. Kwa nini rais alifutlia mbali makubaliano haya yaliyoungwa mkono na majirani zetu wa kusini?

Blinken hakulijibu suala hilo moja kwa moja lakini alisema Rais Joe Biden anadhamira kuona Marekani ina mpaka wenye wa usalama, uopangika na kuheshimu ubinadamu pamoja na Mexico.

XS
SM
MD
LG