Uchunguzi huo utasimamiwa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na tuhuma za uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadam katika jimbo la Tigay kaskazini mwa Ethiopia.
Kundi hilo la kutetea haki za binadam linawatuhumu wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea kushambulia kiholela kwa mizinga mji wa Aksum mwezi Novemba.
Ikitaja ripoti ya wiki iliyopita ya Amnesty International, Human Rights Watch inasema wanajeshi wa Eritrea baadae waliwaua karibu raia 200.
Eritrea hapo awali ilikanusha tuhuma hizo, nayo kamisheni ya haki za binadam ya Ethiopia inasema tuhuma hizo zinabidi kuchukuliwa kwa dhati.
Hapo jana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikuweza kukubaliana juu ya taarifa ya pamoja juu ya ugomvi wa Tgray.