Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:18

Waziri mkuu wa Ethiopia akiri uwepo wa Eritrea, Tigray


Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abby Ahmed, amekiri Jumanne kwamba vikosi vya nchi jirani ya Eritrea viko katika jimbo la Tigray lililokumbwa na mgogoro.

Pia ameeleza kuwa huenda vilihusika na ukiukwaji wa haki dhidi ya raia.

Waziri mkuu Ahmed, alibainisha hayo katika hotuba yake kwenye bunge.

Katika taarifa hiyo ya kushangaza, pia amekubali kwa mara ya kwanza kwamba vitendo vya kinyama kama vile ubakaji vilifanyika wakati wa mapigano, na kuahidi kwamba wote waliohusika watashughulikiwa.

Mapigano yalianza katika jimbo la Tigray, baada ya vikosi vinavyotii chama kilichokuwa kikitawala jimbo la Tigray, Cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kushambulia kambi za jeshi kote katika jimbo hilo usiku, na saa asubuhi za Novemba 4.

Mashambilizi hayo mwanzo yalidhoofisha majeshi ya serekali, ambayo baadaye yalianzisha mashambulizi ya kujibu pamoja na wanajeshi wa Eritrea, na vikosi vya jimbo jirani la Amhara.

TPLF ambayo ilikuwa na ushawishi katika serekali ya Ethiopia kwa kipindi cha takriban miongo mitatu mpaka alipokuja waziri mkuu Abiy madarakani mwaka 2018, na kwa miaka mingi imekuwa adui wa Eritrea.

Abiy amesema vikosi vya Eritrea vilivuka mpaka kwa sababu vilikuwa na wasiwasi wa kushambuliwa na vikosi vya TPLF, lakini Wairitrea waliahidi kuondoka baada ya jeshi la Ethiopia walipofanikiwa kudhibiti mpaka. TPLF mara kwa mara ilirusha makombora Eritrea baada ya mgogoro kuanza.

XS
SM
MD
LG