Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:12

Mashambulizi ya Tigray yatakiwa kusimamishwa


Maandamano ya kutaka kujitenga kwa Tigray
Maandamano ya kutaka kujitenga kwa Tigray

Darzeni ya maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa jana waliomba kusitishwa mara moja kwa mashambulizi holela na kulenga raia katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray, wakitaja pia ripoti za ubakaji na vitendo vingine vya kikatili vya manyanyaso ya ngono.

Katika taarifa ya pamoja, maafisa hao ambao ni mkuu wa misaada kwenye umoja wa mataifa Mark Lowcock, kiongozi wa baraza la haki za binadamu Michelle Bachelet na mkuu wa shirika la wakimbizi Filippo Grandi, wameziomba pande zinazogombana kulinda raia dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu, kulaani manyanyaso ya ngono na kuwawajibisha wahusika.

“Ni muhimu uchunguzi huru kuhusu manyanyaso ya ngono yanayohusiana na mzozo wa Tigray uanzishwe, na kuishirikisha ofisi ya umoja wa mataifa ya Kamishna mkuu wa haki za binadamu”, taarifa hiyo imesema.

Mapigano kati ya wanajeshi wa serekali ya Ethiopia na wapiganaji wa chama tawala cha zamani katika jimbo la Tigray, Tigray people’s Liberation Front (TPLF), yaliuwa ma elfu ya watu na kulazimisha ma elfu ya wengine kukimbia makazi yao katika jimbo hilo la milimani lenye wakazi millioni 5.

XS
SM
MD
LG