Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:57

Misri yatoa tahadhari ya kutokea mgogoro na Ethiopia


Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi
Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, Jumatano ameonya juu ya madhara ya mgogoro unaotokana na bwawa kubwa la uzalishaji umeme la Ethiopia linalotegemea maji ya Blue Nile.

Tahadhari hiyo ya rais wa Misri ameitoa baada ya mazungumzo yaliyo husisha nchi hizo mbili na Sudan kumalizika bila ya muafaka kupatikana.

Ethiopia inaendelea na matarajio ya maendeleo ya uchumi wake, na uzalishaji umeme katika bwawa hilo kubwa, ambalo Misri inahofia litapunguza kiwango cha maji yam to Nile.

Sudan pia ina wasiwasi kuhusu matokeo ya upatikanaji wa maji yake.

Ujumbe kutoka serekali za mataifa hayo matatu ulikutana mapema wiki him mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya Kidemekrasia ya Congo, lakini ulishindwa kuleta matokeo yaliyotarajiwa.

Akizungumza katika uzinduzi wa ukumbi mpya wa serekali, rais Sisi amesema kwamba Sudan na Misri zilikuwa zikiratibu masuala hayo, na kwamba ushirikiano na makubaliano ni muhimu zaidi kuliko chochote.

Akitolea mfano migogoro ya zamani ya kikanda, amesema kwamba wameshuhudia madhara ya migogoro.

Akasisitiza kwa kupeleka ujumbe kwa Ethiopia, kwa kuita ndugu zake, kwamba wasifikie hatua ya kugusa tone la maji ya Misri, kwa kuwa kuna njia nyingi zilizowazi za kufikia muafaka.

Kutokana na hayo waziri wa maji wa Ethiopia Seleshi Bekele ameonekana kupunguza wasiwasi uliopo.

Akizungumza na wanahabari hapo jana, amesema hakuna sababu ya kuingia katika vita kwa sababu ya maji.

Katika ujumbe mfupi wa simu kwenda kwa shirika la habari la Reuters amepinga madai kwamba Ethiopia inatumia maji ya taifa jingine.

XS
SM
MD
LG