Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:23

UN yatoa msaada dola milioni 65 kwa Ethiopia


Wakimbizi wakiwasili katika shule ya msingi ya Tsehaye ambayo ilibadilishwa kuwa eneo la kuhifadhi wakimbizi la muda katika mkoa wa Tigray Ethiopia, March 14, 2021
Wakimbizi wakiwasili katika shule ya msingi ya Tsehaye ambayo ilibadilishwa kuwa eneo la kuhifadhi wakimbizi la muda katika mkoa wa Tigray Ethiopia, March 14, 2021

Umoja wa Mataifa unatoa dola milioni 65 kwa mahitaji ya kibinadamu nchini Ethiopia, kati ya hizo dola milioni 40 zitaenda kwenye operesheni ya misaada katika eneo la kaskazini katika mkoa wa Tigray.

"Hali ya waEthiopia na maisha kwa jumla yanaharibiwa na ukame, na watoto wanaugua utapiamlo," mkuu wa misaada ya Umoja wa Mataifa Mark Lowcock alisema katika taarifa yake.

Alhamisi wakati wa kutangazwa kutolewa kwa fedha hizo. "Na miezi sita katika vita huko Tigray, raia wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Wanawake na wasichana wanalengwa na unyanyasaji wa kijinsia, na mamilioni wanateseka kupata huduma muhimu na chakula, haswa katika maeneo ya vijijini ambayo hayawezi kufikiwa kabisa.

Alisema majibu ya kibinadamu yanahitaji kuongezwa sasa. Zaidi ya watu milioni 16 wanahitaji msaada kote nchini Ethiopia, pamoja na wastani wa milioni 4.5 katika mkoa wa Tigray.

Tigray imekuwa kitovu cha uhasama tangu Novemba, wakati mapigano yalipozuka kati ya Tigray People's Liberation Front (TPLF) na ya serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. Maelfu ya wakazi wa Tigray wamekimbilia Sudan kutoroka mapigano.

XS
SM
MD
LG