Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:06

Mto Nile : Ethiopia yasema itaendelea kujaza maji katika bwawa


FILE - Picha hii ya Julai 20, 2020, na kutolewa na Adwa Pictures Julai 27, 2020, ikionyesha mandhari ya Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance katika Mto wa Blue Nile in Guba, kaskazini magharibi Ethiopia.
FILE - Picha hii ya Julai 20, 2020, na kutolewa na Adwa Pictures Julai 27, 2020, ikionyesha mandhari ya Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance katika Mto wa Blue Nile in Guba, kaskazini magharibi Ethiopia.

Waziri wa Maji wa Ethiopia Seleshi Bekele anasema nchi yake itaendelea na mpango wa kujaza maji bwawa kubwa kutoka Mto Nile jambo ambalo linasababisha ugomvi mkubwa na jirani zake wa Misri na Sudan.

Akizungumza Jumatano Bekele amesema hawatazuiliwa na mtu yeyote katika kukamilisha mradi wao kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hizo tatu.

Ameongeza kusema kwa mwaka wa pili sasa wamekuwa wakijaza bwawa na hakuna athari zilizotokea.

Waziri ameeleza madai ya Sudan kwamba mji wa Khartoum utakuwa na upungufu mkubwa wa maji na karibu watu milioni 20 kando ya Mto Nile watakosa maji ni mambo ambayo hayakutokea.

Ujenzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance umekuwa kiini cha mvutano kati ya mataifa yanayopakana na Mto Nile tangu Ethiopia kuanza mradi huo mwaka 2011.

Duru ya mwisho ya mazungumzo kutanzua mzozo huo ilimalizika Kinshasa Jumanne usiku bila ya kufikiwa makubaliano.

XS
SM
MD
LG